Tuesday, July 14, 2009

UKOSEFU WA CHAKULA UMEZIKUMBA WILAYA NYINGI HAPA TANZANIA

Na Bashir Salum,

Umaskini sio tatizo bali ni changamoto katika maisha haya ni maneno yaliosemwa na mtaalamu mmoja wa mambo ya uchumi kutoka nchi za magharibi

Haya yanatokana na mtu hujifunza kutokana na makosa hivyo umaskini tukiuchukilia kama kosa litatufanya tutafute namna ya kutolirudia kosa

Unaweza kutumia nafasi ya umaskini ulionao ikawa kama changamoto za kimaisha na ukakuletea ubunifu na ukaepukana na umaskini daima

Wanauchumi husema kuwa katika uzalishaji lazima uangalie kiwango cha rasilimali ulichonacho ndipo ufanye uchaguzi sahihi kutokana na rasilimali zilizopo

Ukosefu wa chakula unazikumba wilaya ya nyingi hapa nchini unaweza kuzuiliwa au kutokomezwa kwa kuangalia misingi ya kiuchumi na kimazingira yaani rasilimali zilizopo

Rasilimali zikitumika vizuri sisi watanzania wimbo huu wa uhaba wa chakula ulioanza tangu mimi sijazaliwa ndipo utakapoweza kupata mwitikiaji

Kama uionavyo foleni ya magari katika jiji la Dar es salamu kila kukicha ndivyo ilivyopanga foleni njaa na kujisogeza kidogokigogo katika maisha ya mwanadamu wa kitanzania

Kutokana na ukame unaozikumba wilaya nyingi hapa nchini zinatakiwa mbinu mbadala za kuweza kuhakisha kuwa foleni hii ya njaa toka mwaka 1961 mpaka huko tuendako inapatiwa dawa

Asilimia zaidi ya 80 ya maisha ya mtanzania yanategemea kilimo lakini pia sio lazima asilimia 80 ya chakula cha mtanzania kitokane na kilimo

Zipo sekta nyingine zinazoweza kumfanya mtanzania akapata chakula katika njia tofauti na kilimo kuliko kutegemea kilimo cha kutegemea mvua

Serikali kupitia matawi yake kama wizara ya kilimo inafanya mambo mengi ikiwa ni jitihada zake za kuwaepusha wananchi na matatizo ya ukosefu wa chakula nchini kote

Hii ikiwa ni pamoja na kuanzisha program mbalimbali zikiwa na sura ya (MKUKUTA) yaani mkakati wa kupunguza umaskini japo haijafikia asilimia zilizotzrajiwa

Mbali na jitihada zilizofanywa na serikali lakini Imeripotiwa kuwa mikoa ya Kilimanjaro, Tanga , shinyanga na mkoa wa Mara zimekuwa na matatizo ya upungufu wa chakula

Mkoa wa Singida unahitaji jumla ya ya tani 309 za chakula ili kukidhi angalau kwa kiasi kidogo hali ya mbaya ilijitokeza hivi karibuni

Hayo yalisemwa na mkuu wa mkoa wa Singida Bw Parseko Kone wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya serikali ya mkoa huo kwa waandishi wa habari

Hata hivyo bwana kone alisema kuwa maeneo hayo ambayo yameainishwa yapo katika ukanda wa bonde la ufa katika wilaya ya Manyoni na Iramba

Pamoja na hayo wilaya ya manyoni kuna upungufu wa tani 247zinazohitajika ili kuondoa tatizo la njaa lilowakumba wakazi wa eneo hilo

Katika wilaya ya Iramba ya katika mkoa wa Singida inahitaji tani 62 za chakula na hivyo kufanaya jumla ya tani zinazohitajika kufikia 309

Tukiangalia katika Wilaya ya Same yenye zaidi ya wakazi Wilaya ya Same ambayo inawakazi zaidi ya 244,089 baadhi ya yao wanakumbwa na uhaba wa chakula

Zaidi ya wakazi 30,000 wa kata 15 za wilaya ya Same wanahitaji chakula cha msaada kutoka serikalini

Kwa mujibu wa afisa kilimo na maandeleo ya mifugo na kilimo wa wilaya hiyo Majid Kabyela amesema tani 764 za chakula zinahitajika ili kuwanusuru wakazi hao na baa hilo
Maeneo ya liothirika ni kata ya Mhezi,Myamba, Msindo, Kisiwani Vunta,Hedaru, Suji, Makanya , Vudee, Mwembe, same, Njiro, na Kirangare

Tathimini iliyofanywa septemba mwaka jana ilionesha kwamba wilaya 20 wangeweza kukabaliwa na upungufu wa chakula katika mwezi wa disemba mwaka jana na mwezi huu hivyo kuhitaji tani 7182 za chakula ambacho tayari kilishatengwa kutoka (national food reserve agency) NFRA

Hata hivyo Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (sera uratibu na bunge) Philip Marimo baada ya kutembelea ghala la hifadhi ya chakula la kipawa Dar es salam alisema kuwa baadhi ya wilaya zimeshatengewa fedha ya kuweza kusafirishia chakula hadi vijijini

Moja ya wilaya zilizopata kutengewa hela ya kusafirishia chakula kitakachotolewa na serikali ni Bunda, Iramba, Manyoni, Rombo, Mwanga, Same, Monduli, Ukerewe, Bariadi, Kishapu na Shinyanga vijijini

Wakati huo imeripotiwa katika gazeti la Tanzania daima la tarehe 26 januari kuwa zaidi ya wakazi 300 wa kijiji cha Kalalani wilayani Korogwe wapo hatarini kupoteza maisha kutokana na njaa inayowakabili

Taarifa hiyo ilizibitishwa na serikali ya kijiji cha Kalalani ni kwamba eneo hilo linalokumbwa na janga la njaa na msaada wa haraka unahitajika ili kuhakikisha kuwa maisha ya wakazi hao yananusurika

Hii ikiwa ni moja ya jitihada inayofanywa na serikali kufanya tathimini na kuyatambua maeneo yalio na upungufu wa chakula na ili kuweza kutatua matatizo yalioko

Hata hivyo haya yanaendana na kauli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete alitoa akiwa visiwani Zanziba kuwa hakuna mtu atakaye kufa kutokana na njaa

Mimi tokea nasoma shule ya msingi nilikuwa nikisiki mkoa wa Dodoma kunakuwa na uhaba wa chakula lakini kumekuwa na jitihada za makusudi mji ule

Katika sikuku ya nanenane ya mwaka jana iliyofanyika kitaifa viwanya vya nzuguni mkoani Dodoma mwenyeji alukuwa ni mkuu wa mkoa wa Dodoma bwana Lukuvi

Bwana Lukuvi alisema kuwa mkoa ule unafanya jitihada za hali ya juu kuhakikisha kuwa inatumia rasilimali zake ili kuondokana na kuhakisha kuwa mkoa unajitegema kwa chakula

Enzi za mwalimu ambapo inawezekana mi nilikuwa mdogo lakini nilipata kuelezewa kuwa mwalimu alikuwa mkali sana kwa upande wa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya hasa katika kuwa karibu na maendeleo ya mikoa yao

Moja kati ya hadithi nilizopata kuzisikia ni kuwa mwalimu alishawahi kusema kuwa ‘tunaweza tukafukuza mabwanashamba wote na kilimo kikaendelea kuwa hai’

Kwa kauli hii ya mwalimu ni kwamba inawezekana kuwa mabwanashamba wapo lakini hawafanyi kazi ndio maana hakuna tofauti na wasipokuwepo

Mimi siemi hivyo lakini niseme tu kuwa ni vizuri mabwanashamba kufamu kuwa mkulima anayetegemea kilimo akilia njaa hayo yatakuwa ni mapungufu ya bwanashamba husika

Pamoja na hayo turudi kwenye ukweli kuwa Tanzania inayojivunia mbali tu kilimo lakini bado kuna rasilimali nyingi ambazo zipo na zingeweza kuwa mbadala hasa kwa nia ya kuondoa upungufu wa chakula

Hivi ukifikiria kwa makini mkoa wa Kilimanjaro wenye vivutio vingi, mkoa unaoitambulisha Tanzania duniani mkoa unaunganisha Tanzania na nchi za jirani kama Kenya na ni mkoa wenye misitu midogo na mikubwa lakini eti wanalia njaa?

Ukiangalia mkoa wa Tanga hautataja historia ya Tanzania bila kuutaja mkoa wa Tanga mkoa ulio na bandari na tena mkoa wenye vivutio vya kila aina na ardhi yenye rutuba na unaunganiasha mji muhimu ya Tanzania ikiwemo Dar es salaam na Arusha lakini leo korogwe wanalia njaa!

Ukiangalia mkoa wa Mara nao una utajiri mbali na kuwa una uwezo katika kilimo lakini pia ni mji wa kitalii na kibiashara zaidi
Ni lazima maisha ya mtanzania yaangaliwe kwa jicho la tatu na maisha yasipelekwe ki siasa yawe kivitendo

Kuanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi ya mkoa kuwepo na mshauri katika mambo ya maendeleo na kujihami kutokana na kubadilika kwa hali ya nchi

Kila mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya na halmashauri zake angetakawa kuwa wabunifu na kuweza kuzitambua rasilimali mbalimbali zinazopatikana katika mikoa au wilaya hizo ili kuondokana na aibu hii ya njaa

Angalia mkoa wa Mara,Kilimanjaro,Tanga na hata Singida utagundua kwamba kuna rasilimali kubwa katika mikoa hiyo ambayo ingetumiwa vizuri njaa haitakuwepo

Ni kweli kabisa kuwa tunategemea kilimo lakini kuna sekta nyingine ambazo zinasapoti sekta ya kilimo na zinaweza kuwafanya watu kupata chakula cha kutosha mbali ya kilimo

Lakini hata kutumia zile fursa za ASDPS na DADPS ili kuzindua miradi mingine ambayo itasapot kilimo kwa kupata kipato zaidi bila kuuza mazao yetu ya kilimo

Ili wilaya hizi ziweze kuondokana na foleni ya njaa ni lazima kuwepo na mkakati wa kutumia maligafi zote ambazo zinapatikana ndani ya wilaya hizo badala ya kutegemea kitu kimoja

Hata hivyo Kama kilimo cha umwagiliaji kitapewa kipau mbele kwa maeneo ambayo yanayobahatika kupata maji yanaweza kuondoa tatizo la njaa kwa kuendeleza umwagiliaji

Eidha kupunguza biashara ya mkaa na upasuaji wa mbao kunaweza kusaidia kuondoa tatizo la ukame na njaa kwani uchomaji wa mkaa umechangia kuongezeka kwa ukame katika wilaya ikiwemo same mwanga na zinginezo

Kutilia mkazo vyama vya ushirika nayo ni nyenzo muhimu katika hili kwani ushirika unaweza kutoa huduma za pembejeo , na mikopo na masoko ya mazao kwa wananchi na pia kufanikisha mipango ya maendeleo

Elimu ya ujasiria mali ni muhimu pia kwa watu wa mikoa na wilaya zilizoathirika na baa la njaa kwa sababu sio lazima kutegemea kwenye kilimo na biashara ya mkaa tu bali unaweza kupata elimu ya ujasiria mali waweze kutumia malighafi chache zilizopo kwa manufaa

Mihogo ambayo inapatikana katika wilaya ya Same mwanga na hata baadhi ya wilaya za mkoa wa mara kama elimu ya ujasiria mali itawafikia wanaweza kujua kwamba zao hilo mbali ya ugali unaweza kutengeneza vitu vingine kama chapati, keki tambi na vituvingine ambavyo vingeweza kuondoa umaskini na utegemezi wa kilimo zaidi

Kama Serikali inavyo jitahidi kuanzisha miradi tofauti ya maji na kilimo cha umwagiliaji wilayani wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya waboreshe mali gafi ambazo zipo na zinaweza kuondoa matatizo ya chakula

Kwa yale maeneo kame kuwepo na utumiaji wa maji ya matone mfumo huu unatumia maji kidogo ukilinganisha na umwagiliaji wa mifereji ambao hutumia maji mengi katika kilimo

Naona sasa ifikie mahali iwe ni wimbo wetu wote kwamba wote tulime kilimo cha kisasa,na tutumie zana bora mbegu bora ili kupata kilichobora zaidi

Pamoja na hayo watanzania wote tuamue kufanya kazi tuwe wabunifu kwani matatizo sio kama upepo unavuma ambao mungu anauleta na hakuna binadamu anewezakuusimamisha

Matatizo yote yanaweza kwisha kama watu tukiwa na nia kuwa na moyo wa kujitolea na kuacha siasa katika kazi ila vitendo kwa wingi

Kuna msemo wa china unaosema kwamba ‘kizazi hiki kipande miti ili kizazi kijacho kipate kivuli’ tukiuamini na kuufanyia kazi msemo huu tutaondokana na matatizo kama haya

Hivyo tunatakiwa kujua kuwa hata siku moja Serikali haitamuwekea mtu pesa mifukoni mwake ila imeanzisha SACCOS ambapo mtu unaweza kukopa na kuendeleza shughuli zako

Sasa viongozi wetu ni lazima tutilie mkazo ushirika ilituweze kufaidika kupitia ili kuweza kufaidika kwa hilo

MWISHO

No comments:

Post a Comment