Tuesday, July 14, 2009

MKOA WA KILIMANJARO NJAA KILA WAKATI

Na Bashir Salum

Watu husema umaskini ni sawa na mzigo wa mzoga ambao kama hutautua kwa ajili ya harufu yake basi utautua kwa uzito wake.

Haya ndio yanayowakuta watu watanzania wengi hasa wa Mkoa wa Kilimanjaro ambao wana mzigo wa upungufu wa chakula kwa sababu ya kutegemea mvua za msimu.

Mkoa wa Kilimanjaro unatakiwa kutumia mbinu za ziada ili kuutua mzigo wa upungufu wa chakula unaoikabili mkoa ule hasa wilaya ya Mwanga mara kwa mara .

Upungufu wa chakula unao ukumba mkoa wa Kilimanjaro unaweza kuzuiliwa kwa kuboresha kilimo, ufugaji na kuvitumia vizuri vyama vya kuweka na kukopa.
Vipo vyama vingi vya kuweka na kukopa vilivyoanzishwa na wananchi wenyewe lakini hata wakopaji wamekuwa wakiitumia katika kilimo ambacho nacho hutegemea mvua za msimu

Ni sababu hiyo ya utegemezi wa mvua ndio maana hata mikopo hiyo inakuwa haiwasaidii sana katika kuondoa kawaida ya kuwa na njaa za mfululizo

Kutokana na kutegemea mvua za msimu wakulima mkoani Kilimanjaro wamekuwa wakishindwa kupata mavuno ya kutosha kutokana na uhaba wa mvua ambao kwa kipindi hiki umekuwa ukijitokeza kwa kiasi kikubwa.

Wakulima wadogowadogo inafaa wawe wanatafuta pembejeo za kilimo kulingana misimu waliyonayo mkoani Kilimanjaro.

Naibu waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Dr David mathayo alisema njia inayoweza kumhakikishia mkulima kuwa na uhakika wa chakula katika mikoa ile ni kujikita katika kilimo cha umwagiliaji, uchaguzi wa mbegu bora katika upandaji na kuwa na kawaida ya kuhifadhi chakula

Mbegu za mda mfupi na zenye kutoa mazao mengi pia mazao yanayovumilia ukame kama mihogo na mtama yapewe kipau mbele kwa wakulima wa mkoa wa Kilimanjaro ili yaweze kuondoa upungufu wa chakula

Mkurugenzi wa Idara ya usalama wa chakula , Bwa John Mgodo amesema kuwa mikakati shirikishi imeandaliwa kuhakikisha kuwa chakula kilichopo kinawatosheleza wahitaji hasa mikoainayoweza kukabiliwa na njaa

Wakulima wengi mkoani hapo hutegemea kilimo cha mvua na wachache sana kutegemea kilimo cha umwagiliaji ambacho hupatikana zaidi katika sehumu za tambarare kwa msaada wa maji yatokayo kwenye misitu mbalimbali kama vile shengena, kindoroko na mlima kamwala na ile ya mlima Kilimanjaro

Pia ardhi ya sehemu kubwa ya mkoa huo imechoka sana kutokana na kulimwa kwa mda mrefu bila ya mbolea na hata kuongezeka kwa idadi ya wakazi na shughuli nyingine za kimaisha

Hivi karibuni nilikuwa Mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Mwanga nilikutana na mzee mmoja aitwae Sawaya Mchwangondo Marisa (85) wa Usangi Vuagha aliweza kunieleza yafuatayo

Kumekuwa na utamaduni wa aina yake katika upatikanaji wa mvua na upatikanaji wa mavuno na kutokea kwa njaa hasa katika wilaya ya mwaga

Historia inaonesha kuwa Mkoa wa Kilimanjaro kila mwaka unaoshia na 4 au kugawanyika kwa nne lazima kuwepo na ukame pamoia na njaa ambayo huathiri sana uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro

Mwaka 1964 Mkoa wa Kilimanjaro ulikumbwa na njaa ambayo wakazi wa mkoa huo hususni wapare waliita njaa ya mkebe (nzota ya mngebe) kutokana na vyakula vya msaada kupimwa na chombo kiitwacho mkebe

Mnamo mwaka 1968 ilitokea njaa lakini ilikuwa sio njaa kubwa kuliko ile iliotokeo mwaka 1974 ambayo chakula kilichokuwa kinapatikana ni mihongo na yenyewe ilikuwa inapatikana kwa uchache zaidi

Lakini hata hivyo kuanzia mwaka 1978 hali ya chakula ilikuwa sio nzuri ijapokuwa watu wachache wategemeao kilimo peke yake waliathirika zaidi kutokana na mavuno kupatikana lakini yalikuwa kidogo yasiokidhi haja za wakulima

Mwaka 1984 imeelezwa wazi kuwa upungufu wa chakula ulitokea Mkoani Kilimanjaro ulikuwa ni wa kutisha katika kipindi chote ambacho njaa ilshawahi kutokea

Serikali ya kipi hicho cha mwalim Juliasi Nyerere ulichukua hatua za kuaagiza chakula kutoka nje kilichojulikana kama mahindi ya Yanga (yalikuwa ya njano)


Kwa kipindi hiki Taifa zima halikuwa na chakula cha kutosha hivyo haikuwa mkoa wa Kilimanjaro peke yak e bali mikoa yote iliguswa na tatizo alisema mzee sawaya

Imekuwa kawaida watu wa mkoa huo kuamini kama kila mwaka utakao kuwa unnaishia na nne au nane kwao itakuwa na uhaba wa chakula hivyo mwaka uliopita 2008 kwa ujumla wake mkoa wa Kilimanjaro haukuwa na chakula chakutosha kabisa

Upungufu wa chakula mkoani Kilimanjaro huwa unasababishwa zaidi na ukosefu wa mvua za uhakika katika kipindi kizima cha mwaka na kutokuwa na mikakati ya kuhifadhi chakula.

Hata kiwango cha maendeleo kilichofikiwa na Mkoa wa Kilimanjaro kama ujenzi wa nyumba mashule, hoteli na miundo mbinu bora huwa ni moja ya mambo yanayochangia uharibifu wa mazingira yanayochangia kuchoka kwa aridhi mkoani humo

Kutegemea kilimo cha mkono kwa wananchi wengi mkoani pale ni moja ya sababu zinazofanya kutokea kwa upungufu wa chakula ambao hurudisha nyuma kasi ya maendeleo mkoani hapo.

Wakulima wengi wamekuwa hawatumii mbegu sahihi ambazo hazijahakikiwa na wataalamu kwa ubora hivyo kufanya mkulima kutopata mazao ambayo yangemtosheleza katika maisha yake

Tunasema kuwa hali chakulamtu wa kawaida mkoani humo debe moja la mahindi ni 7000 na 8000 sawa na 350 na 400 kwa kilo

Jitihada za makusudi katika hili ni muhimu zichukuliwe ili kuondokana na matatizo ambayo yanaweza kuwa sio ya lazima kwa kuwa inawezekana

Jitihada inayofanywa na ASDP ya kuwawezesha wakulima kupitia ngazi ya wilaya ya DADPS katika kujenga uwezo wa kujiwezesha

Wananchi wa mkoa huo wanatakiwa kutumia mfuko huo wa ASDP katika kuibua miradi mbalimbali ili aweze kupanua uwigo wa upatikanaji wa chakuala na kufanya maisha kuwa marahisi

Mfano katika vijiji vya kata ya Jipendea ambapo hupata maji kutoka sehemu za milimani ikiwemo Usangi, Ugweno na Kilomeni wangeweza kutumia ile asilimia 75 ya uwekezaji inayotolewa na serikali na wahisani kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji

Ipo haja ya technologia za kilimo utumiaji wa zana za kisasa na utaalamu wa kumwagilia kwa kutumia mabomba kutokana na kutumia maji kidogo

Ijapokuwa kunawafugaji ni wengi mkoani Kilimanjaro lakini wanategemea kilimo zaidi ya ufugaji kutokana na shughuli za mifugo kutouwa na tija

Kiasi hicho hakiwezi kuhudumia mahitaji ya familia kama chakula, mavazi,ada ya shule na kujitibu upatapo magonjwa kwa muda wa mwaka mzima

Mifugo inayopatikana mkoa wa Kilimanjaro haiwezi kuondoa njaa kutokana uhaba, na udhaifu wa mifugo yenyewe

Ukame unapo tokea sehemu husababisha Mazao ya chakula kuwa na bei ya juu, mazao mengine ka mifugo yanashuka bei kutokana na ukosefu wa pesa na malisho kwa mifugo

Kwani ukame husababisha mifugo kufa au kukosa afya hivyo kuuzwa kwa bei ya chini ili kukwepa kuwapoteza kabisa

Hivyo ukame unapotokea sehemu Fulani ,mifugo haiwezi kuondoa njaa kwa sababu hata yenyewe huwa inaathirika na ukame na hivyo soko lake linapungua

Hata hivyo wafugaji wengi wa mkoa wa Kilimanjaro hawajawezeshwa kufuga il kupata manufaa ya mifugo yao lakini wao hufuga kama sehemu ya utamaduni wao

Mifugo yao mingi haipatiwi chanjo za magonjwa na hawana elimu ya ufugaji wa kitaalamu ambao ungewawezesha kupata manufaa ya ufugaji

Ili wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro uondokane na njaa za mara kwa mara mbali ya kushiriki kilimo cha umwagiliaji wanatakiwa kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa ili kupata mitaji na kuboresha mifugo yao ikiwa ni pamoja nakupata chanjo za mifugo yao

Mkoa wa Kilimanjaro ni mojawapo ya Mikoa ambayo ina wasomi wengi kuliko Mikoa mingine wataalamu hawa wanatakiwa kushirikiana na kuwashauri na kutoa utaalamu wao ili kuondoa tatizo hili ambalo limekuwa likijirudia kila mara

Katika Tarafa ya Usangi Mkoani Kilimanjaro msimu wa maharage huvunwa kwa kiasi kikubwa lakini wakulima huyauza, tena kwa gharama ndogo, hivyo Serikali za Mitaa zisimamie uuzaji wa mazao ya chakula kiholela ili kuhifadhi chakula cha akiba

Hata hivyo Mbali ya ushirikishwaji wa wananchi katika kilimo cha umwagiliaji na mikakati mingi ya kuhifadhi chakula kwa ajili ya matumizi ya baadae serikali pia inahakikisha kuwa pembejeo za kilimo, dawa na ruzuku kwa wakulima vinawafikia kwa muda unaotakiwa

Mbali na hali ya chakula ambayo inaonekana kwa mwaka huu haitakuwa nzuri Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliwaambia wananchi wakatia akihutubia wananchi wa unguja na pemba alisema kuwa hakuna mtu atakaye kufaa kwa ajili ya njaa

Hii ni kutokana na ukweli kwamba katika akiba ya taifa yaani yale maghala ya kuhifadhi chakula bado kuna chakula cha kutosha hapa nchini

No comments:

Post a Comment