Monday, July 20, 2009

UBORESHAJI WA KILIMO

Na Bashir Salum

Wengi wetu tumekuwa tukiimba nyimbo lakini uchezaji wake hatujui tunachezaje kwa kuwa hata mlio wa mdundo wa ngoma yake hatuujui

Ni wazi sasa kuwa Wimbo tuliokua tunajifunza wote sasa tumeshaujua na kilichobaki sasa ni kujifunza namna ya kucheza kutokana na vionjo vya wimbo wenyewe ulivyo

Kwa kawaida kila wimbo una uchezaji wake na hivyo kama kila mtu atabadilisha wimbo ghafla basi ni wazi kuwa hata uchezaji nao utabadilika

Kwa kipindi kirefu kidogo wimbo wetu ulikuwa ni ‘vijana kukimbilia mjini’ wakitafuta maisha mazuri na yenye unafuu

Katika hatua hiyo wimbo ule tuliuimba lakini kwa kuwa hapakuwa na ngoma tukajikuta kila mtu anacheza kwa mtindo wake anaoufahamu yeye.

Vijana wakakimbilia mjini wakidai kuwa eti kilimo hakilipi wakidhani mjini ndio maisha bora yaliko


Kila mtu ana fikra zake lakini ni kweli kuwa mjini hakuna maisha yanayoshinda maisha ya kule kijini kama misisngi ya uchumi wa kilimo ikisimamiwa vizuri

Hii ilitokana na kuwa kuhamia mjini kwa vijana wengi kulifanya kilimo kikadumaa na wakulima wengi na wale maisha yao yanayotegemea kilimo wakaanza kubadilisha wimbo

Wakati kilimo kinadumaa lakini hata kikichangiwa na vijana wenye nguvu kukimbilia mjini hivyo kukosekana kwa nguvu kazi mambo yakabadilika na kukatokea kwa nyimbo mbili tofauti na kuanza kuimba ule wa ukitaka maisha mazuri yapo mjini

Vijijni kilimo kinasuasua ! huko mji nako vijana walikimbilia kazi ya kuuza nguo yaani wamachingalakini baadae wakijikuta wakilazimika kuimba wimbo mmoja na askari wa jiji yaani jeshi la mgambo

Wimbo wa mgambo huu sio wa kawaida kwani uliwafanya baadhi wa vijana kuukumbuka ule wa shambani ambao ulikuwa mrahisi hata kuucheza

Baada ya matatizo ya kila mtu kutaka kuimba wimbo wake ndio yaliosababisha watanzania waliowengi kuimba wimbo wa huzuni ijapokuwa hawakuwa wakiupenda

Wimbo huu wa huzuni unaimbwa na yeyote mtu si mtoto wala mkubwa wote wanaweza kuiimba nafikiri ni kwa sababu ya machungu yake

Vijana wazee watoto wakina mama wote wanauimba na kuucheza kwa ufasaha wimbo huu ulijulikana kama upungufu wa chakula

Kwa namna moja au nyingine mimi na wewe pia tuna lazimika kuimba wimbo huu hata kama sio ijapokuwa kuimba tu isingetosha kama hakutakuwa na kucheza wimbo huu

Kwa mara nyingi huwa tunaimba nyimbo ili tujifurahishe kwa maana wimbo huleta faraja moyoni hivyo wimbo unatakiwa kuleta faraja na wala sio kilio au huzuni

Wimbo huu wa upungufu wa chakula kutokana machungu yake ulimpelekea Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania aliponuia kwamba kilimo kikisimamiwa vizuri kitawafanya watanzania kuimba wimbo huku wakicheka badala ya kuimba wimbo huku wanalia

Mbali ya kutangaza bajeti ya kilimo kuongezwa katika mwaka wa fedha ujao lakini Mh. Rais pia alitoa kauli iliyoidhinishwa na bunge kuwa pesa zinazorudishwa kutoka katika akaunti ya madeni ya nje EPA zielekezwe katika kilimo na kwa wafugaji

Kauli ambayo imeanza utekelezaji na matunda ya kauli hiyo yameanza kuonekana kwa wakulima hasa wale wa Morogoro katika vijiji vya mkula na sehemu nyingine

Katika hali ya kukomesha wimbo wa huzuni yaani njaa katika taifa pia mheshimiwa Rais aliwaruhusu wafanya biashara kuingiza chakula kutoka nje bila kutozwa kodi ili chakula kupatikana kwa kiasi kikubwa na kuwafanya watu kununua kwa gharama nafuu

Katika mkutano wake na viongozi wa Wizara ya Kilimo uliofanyika Ikulu hivi karibuni Rais alisema kuwa wafanya biashara wanaruhusiwa kuingiza tani 300,000 bila ushuru wowote ndani ya miezi mitatu

Rais Jakaya Kikwete alisema hayo wakati wa kikao chake cha tathimini ya utendaji katika serikali alipokutana na viongozi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Katika jitihada zake za kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula nchini amewataka watafiti wenye nguvu lakini wamefika muda wa kustaafu kuendelea na kazi

Hatua hiyo ya kipekee inadhihirisha ni jinsi gani watu sasa wamechoshwa na wimbo wa huzuni wa kila siku kila mwaka na kila mahali

Kwangu mimi binafsi naamini kabisa kuwa kwa hatua hizo zingeweza kukibadilisha kilimo na kukifanya kisiwe cha kukimbiwa na vijana ambao kwa kipindi cha nyuma walijazana mjini wakipambana na mgambo wa jiji

Kwa hatua hizo ili ziweze kufanikiwa ni jukumu letu vijana tuache migogoro na mgambo wa jiji tikinyanganyana mashati na maji ya baridi kule mjini , turudi tukawekeze kwenye shamba uwezekana ni mkubwa sana kwa wakulima kufanikiwa

Nchi nyingi duniani ikiwemo china zilianzia kwenye jembe la mkono na katika kilimo cha familia kama Tanzania lakini wao sasa kilimo kimekuwa cha kibiashara kwa kuwa tu kiliweza kushirikisha vijana

Hayo yalisemwa hivi karibuni katika wizara ya kilimo chakula na mkurugenzi mtendaji wa China National Agriculture Development Group Coup Bank bwana Chen Youn

Wakati wakiingia mkataba wa ushirikiano katika kilimo na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ili kuharakisha mapinduzi ya Kilimo nchini Tanzania

Aidha bwana Yuan alisema nchi ya China imejipanga kikamilifu hasa katika kilimo na mifugo ili kuleta maendeleo katika sekta husika

Mkataba huo kati ya wizara ya Kilimo na benki kuu ya china inatuashiria sasa turudi shambani tukalima kwa maana Kilimo sasa kinamuelekeo thabiti

Jitihada za serikali hazikuishia hapo tu lakini kwa kipindi kifupi wizara ya kilimo iliingia mkataba na wizara ya mambo ya ndani na ikihusisha jeshi la magereza na lile la kujenga nchi
Hata hivyo mkataba huo ulifanyika kwa makusudikutokana na wanajeshi kuweza kufanikiwa sana kuzalisha mbegu bora na endelevu

Ni pale Rais alipotembelea viwanja vya Nanenane mkoani Dodoma na kuwashauri wa tafiti wa mbegu wa Wizara ya Kilimo kuungana na wenzao wa jeshi la magereza na lile la kujenga taifa kwa kuwa wao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuweza kubuni na kuendeleza mbegu bora

Zote hizo ni jitihada za serikali za kuhakikisha ule wimbo haumbwi tena katika nchi yetu ijapokuwa umezoeleka masikio na midomoni mwetu

Hata hivyo jitihada za kukiendeleza Kilimo hazikuishia hapo kwa Rais pia Waziri mkuu Mh Pinda mwaka jana alipokuwa katika mkutano na wakulima mjini Morogoro katika hoteli ya BZ alisonesha nia yake ya kuanzishwa kwa benki ya wakulima

Alisitiza ubora wa kuwepo benki ya wakulima kuwa itamuwezesha mkulimakukopa kiasi anachotaka na na kurudisha kwa riba ndogo

Jitihada hizo za Mh. Pinda zimeonekana kuwa na mafanikio makubwa ambapo uanzishwaji wa benki hiyo ya wakulima ipo katika hatua ya mwisho ya kuanzishwa

Inatarajiwa kuwa kufikia mwaka kesho yaan 2010 benki hii itakuwa tayari imekamilika na itaanza kutoa mikopo kwa wakulima kwa riba kidogo

Serikali ya Jamhuri ya watu wa korea kumbe nayo ilisikia ule nyimbo watanzania ambayo wanaimba huku wanacheka lakini wanalia kimoyomoyo

Ubalozi wa Korea ulioamua kuipa Tanzania zzana nyingi za kilimo kwa mkoa wa morgoro wakiwa wanatambua kabisa kuwa morogoro panategemewa kuwa ni ghala la chakula

Serikali ya jamhuri ya watu wa korea ilweza kutoa mashine mbili za kuvunia combine harvestertracto za kupanda mpunga mbili za kuendesha na za kukotwa kwa mikono ikiwa ni pamoja na pampu za maji

Hata hivyo wakorea hao waliweza kutoa matrekta 30 pale mjini morogoro kwa ajili ya kulimia kwa lengo la kuhimiza mapinduzi ya kijani

Msaada huo kutoka katika serikali ya Korea uliopokelewa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Wasira mjini morogoro ulidhihirisha wazi kuwa sasa tunafanya Mapinduzi ya kijani

Jitihada hizo zote ninaamini vijana tukiamua kuachana na vurugu za mgambo wa jiji tukirudi mashambani tutakuwa na wimbo mmoja, tutacheza pamoja na vijana wa kisasa wanasema ‘kitaeleweka’

Ili kuweza kufanikisa haya katika kiwango cha mafanikio nilazima tuanzia kubadilika katika Kilimo cha umwagiliaji kwa maana ya kuachana na kutegemea mvua zetu hizi za msimu

Bila umwagiliaji hakutaweza kuwa na Mapinduzi ya Kilimo na pia wimbo wa njaa utaendelea kuwepo daima hivyo ni jukumu letu mimi na wewe tujiandae kukopa katika asasi tofauti zinazokopesha ili tuwekeze katika Kilimo

Wapo vijana ambao wameweza kunufaika sana kwa kupitia kilimo na kunufaika na sasa wanaendesha maisha yao vizuri
Hata Balozi wa Japani nchini Hiroshi nakagawa alipokuwa akizungumza alipozungumzia kuhusu sekta ya Kilimo hasa cha umwagilaji katika mkutano wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TICAD) aliligusa sana kilimo cha umwagiliaji hasa kwa Tanzania

Alilisitiza kuwa Kilimo cha umwagiliaji ndio kilicholeta mafanikio makubwa nchini kwake ambapo Tanzania ikiaamua kufanya mabadiliko

Mwisho

No comments:

Post a Comment