Monday, July 13, 2009

Matatizo ya waislam hayakuanza leo wala jana

Katika historia uislam uliletwa hasa huku afrika na kuenezwa na waarabu

Pia iliaminika kuwa ulikuwa na nguvu sana kuliko dini nyingine lakini kwa ukweli ni kwamba waarabu walikuwa wafanya biashara wazuri na walikuja na elimu lakini ilikuwa na ni elimu ya dini tu

Baadae ndipo walipokuja wamisionari na dini yao ambayo ndio dini ya kristo

Ujio huu wa wamisionari ulikuja na dini, utawala na elimu ya zaidi

Swala ambalo lilifanikisha kuwamiliki waarabu walikuwa wakisambaza dini ya kiislamu

Hii ilitokana na ukweli kwamba wamisionari hao ndio waliokuwa watawala hivyo kuwa na nguvu sana na kuweza kuzima baadhi ya dola za kisilim

Kutoikea enzi za ukoloni ukristo popote duniani umekuwa ukipata misaada ya kifedha na kimawazo kutoka katika mataifa mbalimbali ili kuimarisha utawala wao

Kwa kuwa kipindi chote hicho wakristo walikuwa ndio watawala hata misingi ya elimu waliishikilia wao hivyo ndio waliokuwa na dhamana ya nani apate elimu na nani asipate

Hivyo utaratibu ulikuwa kwamba usiekuwa mkiristo ukitaka elimu basi uwe mkristo mbali na hivyo elimu hupati

Mbinu hii iliwarudisha sana walikuwa tofauti na wakrito na himaya za wakristo zilipata nguvu sana hadi leo

Katika kuimarisha dini ya wamisionari walitumia sana propaganda katika kupata wadau wengi kutokana na nguvu ya neno propaganda yenyewe ilivyo

Propaganda hizi zilitumika katika kuwatia watu woga hasa katika dini ya upande wa pili na kwa wengi walio amini waliaanza kuona uislam kama dini ya shetani,dini ya watu wasiokuwa na elimu na hata kuiona kuwa dini ya kigaidi

Hali hii imeendelea hadi leo ndio maana utakuta waislam kila wanachotaka kukipata kina kuwa kwao ni shida tupu

Mataifa makubwa yanautambua uislam kuwa ukipewa nguvu basi huenda wakakumbuka shida waliopata hivyo hivyo wakalipiza

Haya hanaasababisha Taasisi nyingi sana za kiislam kuvunjika au kutoendela kwani misaada yote ikitolewa na waislam inaitwa ya kigaidi

Waislam wallitaka kujiunga na NIC ilikuwa shida makinisa yakisimamia kidete sasa waislam wanataka kuanzisha mahakama ya kadhi ambayo ki msingi hii ni kwa ajili ya waislam ili kutafuta haki zao za kiislam lakini hata wasiokuwa waislam wana kataa kwa nguvu mi nafkiri kuwa hapa kuna tatizo

Hivi wewe ungepata nafasi ya kutoa maoni yako kuhusu hili ungesemaje?

No comments:

Post a Comment